Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN, au "namba ya NIDA") inahitajika katika huduma nyingi: kutuma maombi ya kazi kupitia Ajira Portal, kuomba mkopo wa HESLB, kusajili laini ya simu, benki na zaidi. Kama umesajiliwa NIDA lakini hujui namba yako, unaweza kuipata mtandaoni bure kupitia mfumo rasmi wa NIDA.
Jinsi ya kupata namba ya NIDA mtandaoni
- Fungua tovuti rasmi ya huduma za NIDA: services.nida.go.tz.
- Chini ya Self Service (Jihudumie NIDA – Mwananchi), bofya Namba ya malipo na Kupata NIN.
- Chagua Fahamu namba yako (NIN).
- Jaza taarifa zako kama zilivyosajiliwa NIDA:
- Jina la kwanza (First name)
- Jina la mwisho (Surname)
- Tarehe ya kuzaliwa
- Jina la kwanza la mama
- Jina la mwisho la mama
- Andika neno la uthibitisho (captcha) linaloonyeshwa, kisha tuma. Namba yako ya NIN itaonyeshwa kama taarifa zinalingana.
Ushauri: andika majina kama yalivyo kwenye usajili wako wa NIDA (mf. kwenye fomu ya usajili). Tofauti ndogo ya tahajia inaweza kufanya mfumo usikupate.
Kitambulisho kimepotea au kuharibika?
Kupitia huduma ileile ya Jihudumie NIDA, unaweza kuomba namba ya malipo (control number) ya kulipia kitambulisho kipya. Kwa mujibu wa NIDA, gharama ni:
- Tsh 20,000 unapobadilisha kwa mara ya kwanza.
- Tsh 30,000 kwa mara ya pili.
- Tsh 50,000 kwa mara ya tatu au zaidi.
Namba ya malipo hutolewa pia kwa wanaohitaji kubadilisha taarifa zinazohusisha kubadilisha kitambulisho, kwa maelekezo ya maafisa wa NIDA. Huduma hii kwa sasa ni kwa raia wa Tanzania.
Bado hujasajiliwa NIDA?
Usajili hufanyika kwenye ofisi za NIDA za wilaya. Kwa kawaida utahitaji cheti cha kuzaliwa na nyaraka nyingine za uthibitisho wa uraia kama utakavyoelekezwa na ofisi husika. Wasiliana na ofisi ya NIDA iliyo karibu nawe kwa orodha kamili ya nyaraka.
Tahadhari
- Tumia tovuti rasmi pekee (inayoishia na .go.tz). Usimpe mtu yeyote taarifa zako ili akutafutie namba kwa malipo.
- Namba ya NIDA ni taarifa binafsi: usiiweke kwenye maoni (comments) au mitandao ya kijamii.
Soma pia: Ajira Portal: jinsi ya kujisajili | Jinsi ya kuomba mkopo HESLB | Jinsi ya kujikinga na matapeli
Comments
Comments
Post a Comment