Ajira za Polisi Tanzania: Sifa za Mwombaji na Jinsi ya Kutuma Maombi

By

Jeshi la Polisi Tanzania hutangaza nafasi za ajira kwa vijana mara kwa mara, na maombi yote hufanyika mtandaoni. Mwongozo huu unaeleza sifa zilizoainishwa kwenye tangazo la ajira la 2025 na jinsi ya kutuma maombi, ili ujiandae kabla ya tangazo lijalo.

Maombi hufanyika wapi?

Kwa mujibu wa tangazo la 2025, maombi yote hupitia Mfumo wa Ajira wa Jeshi la Polisi (ajira.tpf.go.tz), unaopatikana pia kupitia tovuti ya Polisi. Maombi ya posta, barua pepe au kwa mkono hayapokelewi.

Sifa za mwombaji (kwa mujibu wa tangazo la 2025)

  • Uraia: raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, mwenye wazazi ambao pia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
  • Elimu: wahitimu wa kidato cha nne au cha sita, au wenye shahada, stashahada au astashahada katika fani zilizoainishwa kwenye tangazo.
  • Ufaulu: kidato cha nne daraja la I hadi IV (kwa daraja la IV, alama 26 hadi 28); kidato cha sita daraja la I hadi III.
  • Umri: miaka 18 hadi 25 kwa kidato cha nne, cha sita na astashahada; miaka 18 hadi 30 kwa wenye shahada na stashahada.
  • Urefu: usiopungua futi 5 inchi 8 kwa wanaume na futi 5 inchi 4 kwa wanawake.
  • Afya: afya njema kimwili na kiakili, iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
  • Hali ya ndoa: asiwe ameoa, kuolewa wala kuwa na mtoto.
  • Asiwe ametumia dawa za kulevya, asiwe na michoro ya kudumu mwilini (tattoo), asiwe na rekodi ya uhalifu, na asiwe mwajiriwa wa taasisi nyingine ya Serikali.
  • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Polisi na kufanya kazi popote Tanzania, na aweze kuzungumza Kiswahili na Kiingereza.

Sifa hizi zinaweza kubadilika kila mwaka. Daima soma tangazo jipya rasmi la Jeshi la Polisi kabla ya kuomba.

Nyaraka za kuandaa

  • Namba au kitambulisho cha NIDA. Soma jinsi ya kupata namba ya NIDA mtandaoni.
  • Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono, yenye namba za simu, kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), S.L.P 961, Dodoma, iliyoskaniwa kuwa PDF ili kuiambatisha kwenye mfumo.
  • Vyeti vya elimu na taaluma kulingana na kiwango chako.

Gharama na tahadhari

  • Kwa mujibu wa tangazo, mwombaji hujigharimia mwenyewe katika hatua zote za usaili endapo ataitwa.
  • Kuomba ni bure. Usimlipe mtu yeyote anayeahidi "kukupenyeza" kwenye ajira za Polisi au jeshi lolote. Soma jinsi ya kujikinga na matapeli wa ajira.

Soma pia: Maswali ya usaili na majibu | Ajira za majeshi | Ajira mpya serikalini

✅ Jinsi ya kutuma maombi kwa usalama / How to apply safely
  • Tuma maombi kupitia njia rasmi iliyoelezwa kwenye tangazo hili (Ajira Portal, tovuti au barua pepe ya mwajiri).
  • Usilipe pesa yoyote ili kupata kazi. Mwajiri halali haombi malipo. / Never pay money to get a job.
  • Hakiki tarehe ya mwisho na sifa zinazohitajika kabla ya kutuma maombi.
  • Umeona tangazo la kitapeli au link isiyofanya kazi? Tujulishe hapa.

Comments

Comments

Post a Comment